// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KLUIVERT AFUNGUA KITUO CHA SOKA SHINYANGA, AWANOA STAND UNITED - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KLUIVERT AFUNGUA KITUO CHA SOKA SHINYANGA, AWANOA STAND UNITED - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 12, 2015

    KLUIVERT AFUNGUA KITUO CHA SOKA SHINYANGA, AWANOA STAND UNITED

    Na Philip Chimi, SHINYANGA
    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Ajax Amsterdam, Barcelona ya Hispania na Newecastle ya England, Patrick Kluivert amewasili Shinyanga kwa shughuli mbalimbali za kimichezo ikiwemo kufugua kituo cha michezo katika shule ya sekondari Com mjini hapa.
    Kluveirt ambaye ameambatana na mchezaji wa zamani Real Madrid na Barcerona za Hispania, Marco Garcia walikuwa wageni wa Mbuge wa jimbo la Shinyanga, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Steven Masele wakati wa kufunga kituo cha michezo katika shule ya sekondari com kwa lengo la kutengeneza vijana wazuri wenye uwezo wa  kucheza mpira kwa ufundi zaidi.
    Kluivert akiwa akiwa na wanafunzi wa Com
    Kluivert akiwanoa wachezaji wa Stand United
    Kluivert katikati wakati wa ufunguzi wa kituo hicho

    Akifungua kituo hicho, Steven Masele alisema kituo hicho cha michezo kitatumika kuinua vipaji kwa wachezaji na pia kuwaomba wazazi pamoja na wadau wengine wa soka mkoani shinyanga kushikamana katika michezo.
    “jengo hili ni kwa ajili ya kuweka vifaa vya michezo pamoja na kutoa mafunzo kwa watoto watakao jiunga na kituo hiki ambapo moja ya vifaa hivyo ni gym na vifaa vingine vya mazoezi”alisema Masele.
    Kwa upande wake, Kluveirt alisema kuwepo kwa kituo hicho ni njia pekee ya kuibua vipaji na kutengeneza wachezaji ambao wataweza kucheza mpira vizuri ndani ya nchi na hata nnje ya nchi pia na hivyo kuwataka watoto wanaocheza mpira mjini Shinyanga kutumia fursa hiyo.
    “Mimi nilianza kucheza mpira nikiwa mdogo sana, lakini nilijituma hivyo ukianza mpira ukiwa mdogo utakapo kua utaweza kucheza mpira vizuri sana”alisema  Kluivert.
    Kabla ya zoezi hilo kufanyika Patric Kluivet alianza kwa kuzungumza na kutoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya Stand United ya mjini Shinyanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage.
    “Katika kucheza mpira mchezaji yeyote anatakiwa kuwa na vitu vitatu muhimu kwanza awe na nidhamu, awe msikivu kwa mwalimu wake halikadhalika kujituma katika mazoezi, akifanya hivyo, lazima atafanya vizuri. Hivyo nawaomba msikilize sana mwalimu wenu anawafundisha nini, pia ni lazima mjitambue kuwa mnafanya nini” alisema Kluivert.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLUIVERT AFUNGUA KITUO CHA SOKA SHINYANGA, AWANOA STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top