Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIUNGO Shaaban Kisiga ‘Malone’ amejitoa katika klabu ya Simba SC kutokana na sababu ambazo bado hazijajulikana.
Kisiga alibeba vitu vyake baada ya mechi dhidi ya Mbeya City Jumatano Uwanja wa Taifa na kuwaambia wenzake anaondoka na anazima simu zake zote ili akipigiwa asipatikane.
Katika mchezo huo, ambao Simba SC ililala 2-1 Kisiga alitokea benchi kipindi cha pili kama ilivyo ada yake kipindi hiki chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic.
Siku zote Kisiga amekuwa akitokea benchi na kwenda kubadilisha mchezo, lakini Jumatano wiki hii hakuweza kuisaidia timu kuepuka kipigo cha timu ya Manispaa ya Mbeya.
Mchezaji mwingine mkongwe, Nassor Masoud ‘Chollo’ amepewa ruhusa maalum ya kwenda kutatua mataizo ya kifamilia.
Chollo ambaye siku hiyo alikosa penalti dakika ya mwisho ambayo kama angefunga Simba SC, ilipata sare, mke wake anaumwa na wana mtoto mdogo ambaye anahitaji uangalizi wa kina, wakati nyumbani hawana msaidizi.
Simba SC ilishuka tena dimbani jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Shaaban Kisiga 'Malone' amejiondoa kikosi cha Simba SC |
Mchezaji mwingine mkongwe, Nassor Masoud ‘Chollo’ amepewa ruhusa maalum ya kwenda kutatua mataizo ya kifamilia.
Chollo ambaye siku hiyo alikosa penalti dakika ya mwisho ambayo kama angefunga Simba SC, ilipata sare, mke wake anaumwa na wana mtoto mdogo ambaye anahitaji uangalizi wa kina, wakati nyumbani hawana msaidizi.
Simba SC ilishuka tena dimbani jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment