// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/- - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/- - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 02, 2015

    KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/-

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    KIPA bora wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake, Belina Julius wa Temeke (pichani) amezawadiwa sh. 500,000 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.
    Dk Mukangara alitoa zawadi hiyo baada ya mechi ya fainali ya michuano iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam. Dk Mukangara alikuwa mgeni rasmi kwenye fainali hiyo.
    Temeke ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini baada ya kuilaza Pwani bao 1-0 katika fainali iliyoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni ya Azam.
    Ilala ilifanikiwa kutwaa baada ya kuichapa Kigoma mabao 3-0. Bingwa amepata sh. milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Proin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/- Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top