Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MAPUNGUFU yaliyopo katika kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, yamesababisha wachezaji ambao wanastahili adhabu na kusimamishwa waendelee kucheza.
Beki George Michael wa Ruvu Shooting amethibitika kumfanyia vitendo visivyo vya kiuanamichezo mshambauliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe katikati ya mwezi uliopita, lakini hajachukuliwa hatua yoyote tangu hapo.
Beki huyo hakuonwa na refa wakati anamkaba koo Tambwe, lakini baadaye picha za video zikaonyesha kitendo hicho cha makusudi na kudhamiria.
Baadhi ya kamera za wapiga picha wa magazeti pia zilinasa tukio hilo na kuchapisha- lakini Bodi ya Ligi ilipokutana ikagundua haina nguvu ya kulifanyia kazi hilo kwa mujibu wa kanuni.
Bodi ikaamua kulipeleka suala hilo katika Kamati ya Nidhamu ambayo bado haijakutana hadi sasa na maana yake, mchezaji huyo yuko huru kuendelea kucheza leo timu yake ikiikaribisha Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Beki Juma Said Nyosso wa Mbeya City alinaswa na kamera za wapiga picha wa magazeti akimtomasa sehemu za siri mshambuliaji wa Simba SC, Elias Maguri Jumatano na jana akaichezea timu yake katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi mjini Morogoro.
Na wachezaji wengine wote ambao wamekuwa wakifanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo vinavyostahili adhabu wataendelea kucheza kama hawajatajwa kwenye ripoti ya waamuzi au makamisaa.
Vyama vya soka na bodi mbalimbali duniani, vimekuwa na desturi ya kuchukua hatua za haraka dhidi ya wachezaji wanaothibitika kufanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo.
Mshambuliaji tegemeo wa Chelsea, Diego Costa hakuichezea timu yake ikitoa sare ya 1-1 na Manchester City kwa sababu alikuwa anaanza kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, kufuatia kumkanyaga beki wa Liverpool, Emre Can.
Costa hakupewa kadi katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, lakini ushahidi wa kamera baadaye ulimtia hatiani, amefungiwa mechi tatu mara moja.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo anaamini kanuni za Ligi zinahitaji marakebisho, ili picha za video ziweze kutumika kama ushahidi wa kuwachukulia hatua wachezaji.
“Lakini ili uboreshaji wa kanuni ufanyike, kuna taratibu za kufuatwa, lazima mapendekezo yatolewe, aidha kutoka kwa klabu zenyewe au bodi ya Ligi, kisha yapelekwe katika kikao cha Kamati ya Utendaji yakajadiliwe,”anasema Wambura.

Beki wa Ruvu Shooting, George Michael (kulia) ataendelea kucheza Ligi Kuu licha ya kumfayia vitendi visivyo vya kiuanamichezo Amisi Tambwe wa Yanga SC |
Bodi ikaamua kulipeleka suala hilo katika Kamati ya Nidhamu ambayo bado haijakutana hadi sasa na maana yake, mchezaji huyo yuko huru kuendelea kucheza leo timu yake ikiikaribisha Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Beki Juma Said Nyosso wa Mbeya City alinaswa na kamera za wapiga picha wa magazeti akimtomasa sehemu za siri mshambuliaji wa Simba SC, Elias Maguri Jumatano na jana akaichezea timu yake katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi mjini Morogoro.
Na wachezaji wengine wote ambao wamekuwa wakifanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo vinavyostahili adhabu wataendelea kucheza kama hawajatajwa kwenye ripoti ya waamuzi au makamisaa.
Vyama vya soka na bodi mbalimbali duniani, vimekuwa na desturi ya kuchukua hatua za haraka dhidi ya wachezaji wanaothibitika kufanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo.
Mshambuliaji tegemeo wa Chelsea, Diego Costa hakuichezea timu yake ikitoa sare ya 1-1 na Manchester City kwa sababu alikuwa anaanza kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, kufuatia kumkanyaga beki wa Liverpool, Emre Can.
Juma Nyosso kulia alimtomasa sehemu za siri mshambuliaji Elias Maguri wa Simba SC Jumtano |
Costa hakupewa kadi katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, lakini ushahidi wa kamera baadaye ulimtia hatiani, amefungiwa mechi tatu mara moja.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo anaamini kanuni za Ligi zinahitaji marakebisho, ili picha za video ziweze kutumika kama ushahidi wa kuwachukulia hatua wachezaji.
“Lakini ili uboreshaji wa kanuni ufanyike, kuna taratibu za kufuatwa, lazima mapendekezo yatolewe, aidha kutoka kwa klabu zenyewe au bodi ya Ligi, kisha yapelekwe katika kikao cha Kamati ya Utendaji yakajadiliwe,”anasema Wambura.
0 comments:
Post a Comment