MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur, Harry Kane ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England.
Kane anashinda tuzo ya Januari baada ya kazi nzuri aliyoifanya mwanzoni mwa mwaka 2015, akifunga mabao matano katika michuano yoye, yakiwemo mawili katika ushindi wa 5-3 dhidi ya Chelsea.
Kinda huyo wa umri wa miaka 21 ananukia katika kikosi cha timu ya taifa ya England baada ya kumvutia kocha Roy Hodgson miezi ya karibuni, ambaye amesema atamuita katika kikosi kijacho.
Harry Kane amekuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Januari wa Ligi Kuu ya England
0 comments:
Post a Comment