// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAGERA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAGERA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Sunday, February 15, 2015

        KAGERA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU

        BAO pekee la mshambuliaji Atupele Green (pichani kushoto) leo limeipa ushindi wa 1-0 Kagera Sugar dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
        Kwa ushindi huo, Kagera ya Bukoba inayotumia Uwanja wa kuhamia baada ya Kaitaba kuwa matengenezoni, inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda hadi nafasi ya tatu, ikiishushia nafasi ya nne Simba SC. 
        Mapema jioni ya leo, Simba ilipaa hadi nafasi ya tatu kwa muda kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya leo.
        Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, washambuliaji Ibrahim Salum Hajibu na Elias Maguri, moja kila kipindi.
        Hajibu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwainua mashabiki wa Simba SC baada ya kumalizia vizuri mpira wa kurushwa na beki Hassan Kessy dakika ya 14.
        Kipindi cha pili, Maguri aliihakikishia Simba SC kutimiza pointi 20 baada ya mechi hiyo ya 14 kwa kufunga bao la pili dakika ya 71.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry