// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JOHN BOCCO MTANZANIA PEKEE ALIYEFUNGA BAO MECHI ZA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JOHN BOCCO MTANZANIA PEKEE ALIYEFUNGA BAO MECHI ZA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 16, 2015

    JOHN BOCCO MTANZANIA PEKEE ALIYEFUNGA BAO MECHI ZA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MTANZANIA mmoja tu amefunga bao katika mechi za kwanza Raundi ya Awali michuano ya Afrika zilizochezwa wikiendi hii, naye ni John Raphael Bocco.
    Timu mbili za Tanzania zimepata ushindi katika mechi zake za kwanza za Raundi ya Awali michuano ya Afrika, lakini wachezaji wa Burundi ndio waliozisaidia sana.
    Yanga SC walianza kuifunga BDF XI ya Botswana mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi yote yakifungwa na Mrundi, Amisi Tambwe kabla ya jana mabao ya Mrundi mwingine Didier Kavumbangu na mzalendo John Bocco kuipa Azam ushindi wa 2-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini.
    John Bocco kulia akipongezana na Didier Kavumbangu jana Chamazi

    Sasa, timu hizo za Bara zitatakiwa kwenda kulazimisha sare ugenini wiki ijayo ili kufuzu 32 Bora ya michuano ya Afrika.
    Wawakilishi wa upande wa pili wa Muungano wa Tanzania katika michuano ya Afrika, KMKM na Polisi za Zanzibar wote walianza vibaya jana baada ya kufungwa ugenini.
    KMKM ilifungwa mabao 2-0 na Al-Hilal ya Sudan mjini Khartoum katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Polisi ilichapwa mabao 5-0 na CF Mounana nchini Gabon katika Kombe la Shiriksiho, zote zikiwa mechi za kwanza Raundi ya Awali michuano hiyo.
    KMKM sasa itatakiwa kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo visiwani Zanzibar, wakati Polisi inatakiwa kushinda 6-0 ili zifuzu hatua ya 32 Bora.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JOHN BOCCO MTANZANIA PEKEE ALIYEFUNGA BAO MECHI ZA KWANZA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top