MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, James Rodriguez juzi ameanza kutembelea magongo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wake wa na anatarajiwa kuwa nje kwa miezi miwili.
Japokuwa klabu yake haijasema atakuwa nje kwa muda gani, lakini taarifa za ndani zinasema mchezaji huyo atakosekana kwa miezi miwili.
Rodriguez aliumia goti baada ya kuifungia bao la kuongoza Real Madrid katika ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Sevilla Uwanja wa Santiago Bernabeu na akatolewa kipindi cha kwanza baada ya madaktari kusema kwamba ameumia sana.
James Rodriguez pichani baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Murcia
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, Rodriguez amefanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza Real chini ya kocha Carlo Ancelotti, baada tu ya kusajiliwa msimu huu kufuatia kuifikisha timu yake ya taifa Colombia, katika Robo Fainali Kombe la Dunia hadi kuibuka mfungaji bora.
Amecheza mechi 33 kati ya 36 za Real Madrid msimu huu, akifunga mabao 12 na kusaisia upatikanaji wa mabao 10 zaidi.
0 comments:
Post a Comment