// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IVORY COAST WATINGA FAINALI AFCON, KONGO WAFA 3-1 BATA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IVORY COAST WATINGA FAINALI AFCON, KONGO WAFA 3-1 BATA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 05, 2015

    IVORY COAST WATINGA FAINALI AFCON, KONGO WAFA 3-1 BATA

    TIMU ya taifa ya Ivory Coast imekata tiketi ya kucheza Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015 kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Bata, Equatorial Guinea usiku huu.
    Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Yaya Toure, Gervinho na Serge Wilfried na sasa Tembo wanakwenda fainali kwa mara ya tatu ndani ya miaka tisa.
    Ivory Coast ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure dakika ya 20, kabla ya Dieumerci Mbokani kuisawazishia DRC kwa penalti dakika ya 24, kufuatia Eric Bailly kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.


    Yaya Toure akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza leo mjini Bata

    Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho akaifungia Ivory Coast bao la pili dakika ya 41, kabla ya Kanon kufunga la tatu dakika ya 68.
    Sasa, mabingwa hao wa mwaka 1992 watashuka dimbani Jumapili kumenyana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho, kati ya wenyeji, Equatorial Guinea na Ghana.
    DRC itawania nafasi ya tatu dhidi ya timu itakayofungwa kesho.
    Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa; Gbhouo, Kanon, Toure, Bailly, Aurier, Tiene/Diarassouba dk72, Toure, Die, Gradel/Kalou dk62, Gervinho na Bony/Traore dk90+2.
    DRC; Kidiaba, Mpeko, Kassusula, Zakuani, Kimwaki, Mbemba, Makiadi/Ndombe dk79, Mabwati/Kebano dk69, Bolasie, Bokila na Mbokani/Kabananga dk61.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST WATINGA FAINALI AFCON, KONGO WAFA 3-1 BATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top