// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HILI LINATAKA KUWA TATIZO SUGU YANGA, PLUIJM NA MKWASA VIPI? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HILI LINATAKA KUWA TATIZO SUGU YANGA, PLUIJM NA MKWASA VIPI? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    HILI LINATAKA KUWA TATIZO SUGU YANGA, PLUIJM NA MKWASA VIPI?

    TATIZO la kutotumia vyema nafasi za kufunga mabao jana limeendelea tena kwa timu ya Yanga SC, ikishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Mashabiki wa Yanga SC jana walishangilia mara mbili, baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Joselyn Tambwe kufunga bao moja kila kipindi katika ushindi wa 2-0, ingawa wangeweza kushangilia hata mara tano kama wachezaji wa timu hiyo wangetumia nafasi nyingi.
    Tatizo nini Yanga SC, wachezaji wanakosa kosa mabao ya wazi? Haijulikani, ingawa unaweza ukasema kwamba tatizo linaenda likipungua, lakini si kwa kasi ya kuridhisha.

    Baada ya ushindi huo wa kawaida jana Uwanja wa Taifa, Yanga SC itasafiri Gaborone wiki ijayo kwenda kuyalinda mabayo hayo, ili ifuzu hatua ya 32 Bora, ambako itamenyana na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimbabwe.
    BDF hawakuwa wanyonge sana uwanjani jana, walijaribu kushambulia kila walipopata nafasi na mara mbili walikaribia kufunga- na haijulikani watakapocheza mbele ya mashabiki wao hali itakuwaje.
    Kipigo cha mabao 2-0 ugenini kwa kweli hakiwezi kumkatisha tamaa yeyote kati ya Watswana- watakwenda uwanjani kwa wingi wiki ijayo kuishangili timu yao.
    Wengi tunatambua na kuheshimu uwezo wa makocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa, lakini bado haiwezi kutuzuia kuweka bayana hisia zetu juu ya kazi yao.
    Tatizo la wachezaji wa Yanga SC kukosa mabao ya wazi, tena mno lilianza tangu Januari wawili hao walipoanza kazi Jangwani wakirithi mikoba ya Wabrazil, Marcio Maximo na Leonardo Leiva.
    Mechi za mwanzoni walianza kwa kishindo wakishinda ‘nne nne’ na magazeti yakaandika “Yanga sasa wamekuwa watamu’.
    Ghafla tu, hali ya ukosaji mabao ya wazi ikaanza kujitokeza katika timu, ikatolewa mapema Kombe la Mapinduzi, wakarudi katika Ligi Kuu ambako na kwenyewe wamekuwa wakishinda kwa tabu.
    Ushindi mnono zaidi wa Yanga SC sasa umekuwa mabao 2-0. Wachezaji wote wanakosa mabao. Tena ya wazi.
    Ikitokea siku mchezaji akaingizwa kutokea benchi na kufunga, mechi ijayo anaanzishwa, lakini hafungi tena.
    Tuliona Danny Mrwanda alifunga dhidi ya Polisi mjini Morogoro, mechi iliyofuata akaanzishwa hakufunga. Mrisho Ngassa alifunga mabao yote mawili dhidi ya Mtibwa Sugar, jana akaanzishwa hakufunga.
    Na jana Tambwe kafunga mabao yote, najua mchezo ujao ataanzishwa tutaona kama atafunga tena.
    Yanga SC inacheza vizuri kuanzia nyuma, inashambulia mno, inatengeneza nafasi nyingi, lakini umaliziaji umekuwa mbovu sana.
    Mabao aliyofunga Tambwe jana, yote ni uzembe wa mabeki wa BDF na kipa wao, kumuacha Mrundi huyo achupie mpira peke yake.
    Yanga kama inakutana na timu yenye ukuta imara, ndiyo maana yake hawawezi kupata mabao. Ukweli ni kwamba, makocha wa Yanga wanapaswa kuketi chini na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo.
    Imekuwa muda mrefu na kasi ya kuliondoa ni ndogo, wakati timu imeingia kwenye michuano ambayo inahitaji umakini wa hali juu.
    Tunaheshimu uwezo wa Pluijm na Msaidizi wake Mkwasa, lakini tatizo la kukosa kosa mabao ya wazi linataka kuwa sugu sasa katika Yanga SC, walitafutie dawa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HILI LINATAKA KUWA TATIZO SUGU YANGA, PLUIJM NA MKWASA VIPI? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top