// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HARRY REDKNAPP ABWAGA MANYANGA QPR BAADA YA KUWA 'MLEMAVU' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HARRY REDKNAPP ABWAGA MANYANGA QPR BAADA YA KUWA 'MLEMAVU' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 03, 2015

    HARRY REDKNAPP ABWAGA MANYANGA QPR BAADA YA KUWA 'MLEMAVU'

    KOCHA Harry Redknapp amejiuzulu Queens Park Rangers baada ya kumpigia simu Tony Fernandes Saa 11:30 jioni.
    Redknapp, mwenye umri wa miaka 67, amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuambiwa anahitaji magoti mbadala ya miguu yake yote miwili, kulia na kushoto. Akiwa hawezi kutembea hata mita 100, amekiri si mtu mwafaka kuiongoza Rangers ambayo iko katika hatari ya kushuka daraja. Amempigia mmiliki Fernandes ndani ya saa chache kumpa habari hiyo.
    "Nimekesha usiku kucha, nafikiria juu ya hilo," amesema Redknapp. "Nataabika mno hivi sasa. Siwezi kutembea, naweza kujitutumua kusimama na kuangalia. Nina maumivu muda wote,"amesema.
    Harry Redknapp quit QPR with the club second bottom of the Premier League
    Harry Redknapp ameachia ngazi QPR huku timu hiyo ikiwa inashika nafasi ya pili kutika mkiani katika Ligi Kuu ya England
    Reknapp on crutches during pre-season
    Redknapp on crutches last season

    Redknapp amesema matatizo ya miguu yake ndiyo sababu ya msingi yeye kuachia ngazi QPR kwa sababu hawezi tena kutembea.
    "Niliomba tiketi ya kwenda kwenye mechi ya Kombe la FA kati ya Fulham na Sunderland Jumanne usiku, lakini mawazo yangu ya kwanza ilikuwa, nawezaje kufika uwanjani? Hata nikipata tiketi ya kuingiza gari, bado kutakuwa na kutembea. Siwezi kutembea Uwanja wa Craven Cottage tena, siwezi kutembea mitaani – huo ndiyo ubaya wenyewe,"amesema.
    "Nilikwenda kumuona mjukuu wangu anacheza soka wikiendi, na baada ya dakika tano ilibidi nirudi kwenye gari. Sikuweza hata kusimama. Maisha gani haya ikiwa huwezi kuwaangalia watoto wanacheza mpira? Hivyo, hilo ndilo lilifanya nifikirie hivyo. Nilikwenda kitandani nikifikiri nitalala, lakini sikuweza kulala. 
    Hivyo nikaamua kumpigia Tony. Ilikuwa majira ys saa 11.30 jioni. Nikamuambia anahitaji mtu mwingine anayeweza kuifundisha na kuiongoza sawia timu katika wiki nyingine 10. Huu ni wakati muhimu, wanahitaji mtu ambaye anaweza kujitolea kila kitu," amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HARRY REDKNAPP ABWAGA MANYANGA QPR BAADA YA KUWA 'MLEMAVU' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top