Na Prince Akbar, DAR E SALAAM
BEKI na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' amemshusha presha kocha wa timu hiyo Hans van der Pluijm baada ya kuthibitika kwamba sasa yuko fiti kwa asilimia 100 kwa mchezo wa kesho.
Yanga SC itakuwa mwenyeji wa BDF XI ya Botswana katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari uliowahusisha makocha wa timu za Yanga na BDF zitakazoshuka uwanjani kesho Pluijm amesea wapo tayari kupambana na Wanajeshi hao lakini furaha yake ni kuwa sawa kwa Cannavaro.
Pluijm amesema wanajua kwamba wanakutana na BDF ambapo wamejipanga kupambana nao kwa nguvu lakini pia watakuwa makini kuhakikisha nyavu zao hazitingishwi na wageni hao.
"Ukisikia nahodha wa tyimu yao anavyosema utagundua kwamba hii timu imejiandaa vya kutosha kupambana na sisi,wanasema wanajua kwamba hapa kuna hali ya hewa tofauti na kwao Botswana lakini wapo tayari kwa lolote na hivyo ndivyo wanajeshi wanavyojiandaa,"alisema Pluijm.
Naye Kocha Mkuu wa BDF Letang Kgengwenyane ametamka kwamba tofauti na timu zingine zinavyocheza ugenini wao wamekuja kupambana kusaka ushindi na hawatajilinda kutafuta sare.
"Imezoeleka kwamba timu inapocheza ugenini inatumia mfumo wa kujilinda, kwetu ni tofauti tutashambulia kwa nguvu lakini pia tutazuia, tunataka kusinga mbele ni lazima tupate mabao,tumefanya maandalizi ya kutosha tangu tulipopata nafasi ya kushiriki kombe hili,"alisema Kgengwenyane.

Cannavaro akiwa Dk Sufiani Juma mazoezini |
Makocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm kulia katika Mkutano wa Waandishi wa Habari akiwa na Kocha wa BDF Letang Kgengwenyane kushoto na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto katikati |
Pluijm amesema wanajua kwamba wanakutana na BDF ambapo wamejipanga kupambana nao kwa nguvu lakini pia watakuwa makini kuhakikisha nyavu zao hazitingishwi na wageni hao.
"Ukisikia nahodha wa tyimu yao anavyosema utagundua kwamba hii timu imejiandaa vya kutosha kupambana na sisi,wanasema wanajua kwamba hapa kuna hali ya hewa tofauti na kwao Botswana lakini wapo tayari kwa lolote na hivyo ndivyo wanajeshi wanavyojiandaa,"alisema Pluijm.
Naye Kocha Mkuu wa BDF Letang Kgengwenyane ametamka kwamba tofauti na timu zingine zinavyocheza ugenini wao wamekuja kupambana kusaka ushindi na hawatajilinda kutafuta sare.
"Imezoeleka kwamba timu inapocheza ugenini inatumia mfumo wa kujilinda, kwetu ni tofauti tutashambulia kwa nguvu lakini pia tutazuia, tunataka kusinga mbele ni lazima tupate mabao,tumefanya maandalizi ya kutosha tangu tulipopata nafasi ya kushiriki kombe hili,"alisema Kgengwenyane.
0 comments:
Post a Comment