AKIWA amecheza kwa zaidi ya muongo mmoja Ulaya, hapana shaka ni sahihi kusema Xabi Alonso anamjua mchezaji mzuri.
Akiwa ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ametaja kikosi cha wachezaji 11 bora wa muda wote katika zama zake wa Ligi ya Mbingwa Ulaya kwa mtazamo wake.
Kwa sasa akiwa anachezea Bayern Munich, Mspanyola huyo amemteua kipa wa timu yake, Manuel Neuer kuwa mlinda wa kikosi, ambacho ndani yake kuna washambuliaji Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Kikosi kamili cha Alonso ni; Manuel Neuer, Philip Lahm, Sergio Ramos, Carles Puyol, David Alaba, Zinadine Zidane, Paul Scholes, Xavi, Steven Gerrard, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Alonso akifurahia na Mwandishi wa Sportsmail, Jamie Carragher mapema msimu huu Ujerumani
0 comments:
Post a Comment