// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GHANA YAIBABUA GUINEA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GHANA YAIBABUA GUINEA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2015

    GHANA YAIBABUA GUINEA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI

    MABAO mawili ya Christian Atsu yameisaidia Ghana kushinda 3-0 dhidi ya Guinea katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika Uwanja wa Malabo leo.
    Atsu alifunga mabao yake katika dakika za nne na 61, wakati bao lingine la Black Stars lilifungwa na Kwesi Appiah dakika ya 44.
    Kipa wa Guinea Naby Yattara alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90+4 baada ya kumuangusha Asamoah Gyan kwenye boksi.
    Kikosi cha Ghana kilikuwa: Razak Braimah, Harrison Afful, John Boye, Baba Rahman, Jonathan Mensah, Mubarak Wakaso, Afriyie Acquah/Mohammed Rabiu dk85, Christian Atsu/Frank Acheampong dk79, Andre Ayew, Asamoah Gyan na Kwesi Appiah.
    Guinea: Naby Yattara, Baissama Sankoh, Djibril Tamsir Paye, Fode Camara, Abdoulaye Cisse, Aboubacar Fofana, Kevin Constant/Naby Keita dk56, Ibrahima Conte, Ibrahima Traore, Idrissa Sylla/Mohamed Yattara dk45 na Abdoul Razzagui Camara/Francois Kamano dk81.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GHANA YAIBABUA GUINEA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top