MMILIKI wa taji la ngumi za kulipwa duniani la uzito wa Super Middle, linalotambuliwa na bodi ya WBF, Francis Boniface Cheka Jumatatu wiki hii (Februari 2, 2015) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na faini ya Sh. Milioni 1.
Mahakama mjini Morogoro imempa adhabu hiyo Cheka, baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa Meneja wa Baa yake ya Vijana Social mkoani Morogoro.
Baada ya hukumu hiyo, Cheka, aliyezaliwa Aprili 15, mwaka 1982 mjini Dar es Salaam, alidai kwamba sababu halisi ya kifungo chake ni fitina za viongozi wa mkoa wa Morogoro baada ya kudai zawadi yake aliyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete ya bati.
Cheka aliwaambia Waandishi wa Habari akiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa gerezani kwamba, kilichomponza hadi kufungwa ni kudai bati alizoahidiwa na Rais Kikwete.
Cheka alikwenda hadi Bungeni, Dodoma baada ya kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBF, akimshinda Mmarekani, Phil Williams Agosti 30 mwaka 2013 ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kupeleka mkanda huo, ambao Wabunge waliupokea kwa furaha.
Na badaaye, Rais Kikwete kwa kufurahishwa na uwakilishi mzuri wa mbabe huyo kwenye mchezo, akamuahidi bati za ujenzi, huku akiwaagiza viongozi wa Morogoro kulishughulikia hiyo.
Lakini sasa mambo yote ya Cheka yatasimama kwa miaka mitatu akiwa anatumikia kifungo chake jela.
Cheka anakwenda jela tayari akiwa na umri wa miaka 33, maana yake hata kwenye ndondi ndiyo alikuwa analekea ukingoni.
Utarajie nini baada ya Cheka kutoka jela akiwa amefikisha umri wa miaka 36, iwapo hatabahatika kushinda rufaa, au kupata msamaha wa Rais, kama si kusema anakwenda kumalizia ubabe wake gerezani?
Akimaliza kifungo cha miaka mitatu jela na akataka kuendelea kupigana, itakuwa ni zamu yake kupigwa pigwa, kwa sababu atakuwa amekwishachoka.
Hili ni pigo kubwa kwenye maisha ya Cheka, lakini pia na kwa taifa, limempoteza balozi mzuri katika michezo kwa wakati huu. Na baada ya Cheka, nani bondia mwingine anainukia vizuri ambaye atarithi mikoba yake?
Ngumi zenyewe siku hizi nchini zimepoteza mwelekeo, hakuna mapromota wenye maarifa ya kibiashara walio tayari kuwekeza kwa mabondia katika kuwaandaa kama walivyokuwa wakifanya akina Malinzi enzi zao, Philemon Kyando ‘Don King’ au marehemu Peter Timona.
Akina Malinzi kupitia kampuni yao ya DJB Promotions waliwasaidia sana ndugu Mbwana na Rashid Matumla hadi wakapata mafanikio makubwa katika ndondi, wakati Kyando alimsaidia Stanley Mabesi ‘Ninja’ na Timona aliwasaidia Adam Abdulrahman (marehemu) na Shaaban Mohamed ‘Star Boy’.
Mapromota wa leo wanataka bondia aliye tayari ampandishe ulingoni, ndiyo maana kwa muda mrefu jina limekuwa moja tu linalotamba katika mchezo, Cheka tu.
Hali yenyewe ngumu ya maisha hivi sasa utarajie bondia ajiandae mwenyewe kuwa katika kiwango cha ubora wa kimataifa, ni vigumu. Vijana wanahitaji kusaidiwa.
Akina Kyando, Malinzi na marehemu Timona, waliwekeza fedha kwa kuwaandaa mabondia, baadaye wakawa wanajilipa walipoandaa mapambano yaliyovutia watu wengi kutokana na ubora wa wapiganaji wao.
Na bado hawa watu walikuwa wanawasaidia hata mabondia wengine waliovutiwa nao, ili mradi wakuze viwango vyao, kwa kujua siku moja watakuja kunufaika nao.
Ndiyo maana siku za nyuma ndondi zilikuwa raha, wababe wengi, ukienda Tanga kule Mambeya Bakari na marehemu Magoma Shaaban.
Maneno Oswald, Joseph Marwa, George Sabuni, Ernest Bujiku ‘Tyson’, Rashid Matumla, Mambeya Bakari wote walikuwa wanapigana uzito mmoja, walikuwa katika kiwango cha kimataifa na walitamba wakati mmoja, miaka ya 1990.
Ndiyo maana ninasema Cheka kwenda jela ni pigo kubwa katika mchezo wa ndondi na bahati mbaya kwake, amepewa hukumu nzito tofauti na wenzake waliowahi kufanya makosa ya aina hiyo.
Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, aliyewahi kuwika Yanga SC, James Tungaraza ‘Boli Zozo’, sasa marehemu, mwaka 1997 alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa kama la Cheka tu.
Tungaraza aliyechezea pia Vaal Proffessionals ya Afrika Kusini, alimpiga mama muuza chapati aliyekwenda kuwagongea asubuhi kudai fedha zake na alipotoka jela baada ya kumaliza kifungo chake, siku chache baadaye akafariki dunia.
Mwanamuziki Msafiri Kondo ‘Solo Thang’ alihukumiwa kifungo cha nje miezi sita baada ya kumpiga mwanamuziki mwenzake, Zainab Lipangile ‘Zay B’.
Khalid Mohammed ‘TID’ alifungwa mwaka jela (2008) baada ya kumpiga mtu, lakini yeye ilionekana amepewa kifungo kirefu kwa sababu ilidaiwa mtu aliyemshambulia, alikuwa ni mtumishi wa idara nyeti ya serikali. TID hakumaliza, kifungo baada ya kupata msamaha wa Rais Jakaya Kikwete.
Na hata kwa raia wengine, makosa ya aina hiyo adhabu zake zimekuwa ni hizo hizo, kifungo kirefu miezi sita, wenye bahati zao wengine wanaishia kutozwa faini tu.
Hata kwa nchi nyingine zilizoendelea, makosa ya kushambulia hayana kifungo kirefu jela, na wengine wanapewa kifungo cha nje tu.
Bondia Mmarekani, Floyd Mayweather Jr, Juni 1, mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Josie Harris. Hata hivyo, baada ya kutumikia kifungo chake kwa miezi miwili, akaachiwa huru Agosti 3, mwaka huo.
Cheka amekuwa na bahati mbaya sana, kosa kama lake wengine wanapewa adhabu ndogo, lakini yeye miaka mitatu jela!

0 comments:
Post a Comment