KLABU ya West Ham imepigwa faini ya Pauni 71,000 na FIFA baada ya kumtumia Diafra Sakho katika mechi ya Kombe la FA siku 18 tangu ajitoe kikosi cha Senegal kilichocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Sakho alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 Uwanja wa Ashton Gate dhidi ya Bristol City na bodi hiyo ya soka duniani ikaanza kufanya uchunguzi kama walivunja sheria za majukumu ya kimataifa ya mchezaji.
The Hammers walikanusha kufanya jambo lolote baya, wakisema mchezaji huyo alikuwa ana maumivu ya mgongo wakati anaitwa Senegal na akashindwa kujiunga na kikosi, lakini haikuwasaidia kuepuka rungu la FIFA.
West Ham imeadhibiwa kwa kumchezesha Sakho aliyegoma kujiunga na timu yake ya taifa
Senegal ilikasirishwa na kitendo cha Sakho kuichezea West Ham saa 48 baada ya kutolewa kwao kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment