// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); EL MERREIKH WATUA KWA MACHALE DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE EL MERREIKH WATUA KWA MACHALE DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 13, 2015

    EL MERREIKH WATUA KWA MACHALE DAR

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha El Merreikh ya Sudan kimewasili jana mchana tayari kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji Azam FC
    Msafara huo wa El Merreikh umewasili salama  tayari kwa mchezo huo wa Jumapili huku ukiwa na mastaa wake wote wakiwemo Mkenya Allan Wanga na mshambuliaji wa Mali Mohamed Traore.
    Hata hivyo El Merreikh walikutana na kasheshe la kuchelewa Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kufuatia uongozi wa timu hiyo kuwa na mapungufu ya hati zao za kuingia nchini kabla ya Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Rafael Matola kuwaokoa.
    Mshambualaji wa Merreikh raia wa Mali, Mohammed Traore kushoto akiwa na wenzake baada ya kuwasili 

    Baadhi ya wachezaji na viongozi wa El Merreikh wakiwa uwanja wa ndege.

    Timu hiyo iliondoka uwanjani hapo majira ya saa 10 jioni na kuelekea hotelini kwao Serena ambapo ndipo walipojilipia. 
    "Kuchelewa kwao huko hakuwahusu Azam wala TFF, hawa ni kama hawakujiandaa vyema, walikuwa na dosari katika suala la uhamiaji lakini washukuru yule jamaa wa TFF lakini Azam wajiandae na hili hawa wanaweza kuona wenyeji wao ndiyo wamewafanyizia,"alisema mmoja wa maofisa atakayekuwa wenyeji wa Merreikh hapa nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EL MERREIKH WATUA KWA MACHALE DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top