Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, El Merreikh ya Sudan wanatarajaiwa kuwasili leo Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza, Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki dhidi ya wenyeji, Azam FC.
Merreikh wanakuja Dar es Salaam wakitoka kushinda mabao 2-0 Jumapili dhidi ya Hilal El-Fasher katika Ligi ya Sudan na kwa ujumla wamepoteza mechi moja tu kati ya 36 walizocheza tangu Februari 11, mwaka jana.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya Kundi C, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda Agosti mwaka jana.
Ukiondoa Kagame, katika mashindano makubwa mara ya mwisho Merreikh ilifungwa na KCCA ya Uganda katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2-0 Februari 8, mwaka jana katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali uliofanyika Sudan.
Mchezo wa marudiano, Merreikh ilishinda 2-1 Kampala, lakini wakatolewa.
Mchezo huo utakaofanyika Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam utachezeshwa na refa Hassan Mohamed Hagi, wasaidizi wake namba moja Bashir Sh Abdi Sule na namba mbili Salah Omar Abubakar wakati mezani atakuwa Kidane Melles Terfe, wote wa Somalia.
Kamisaa wa mchezo huo atakuwa M.CHaileyesus Bazezew Beleti kutoka Ethiopia.
Azam FC na Merreikh zilikutana mara ya mwisho Agosti 20, mwaka jana katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda. Dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na katika mikwaju ya penalti Merreikh ikashinda 4-3.
Siku hiyo, penalti za Azam zilifungwa na Erasto Nyoni, Didier Kavumbagu na Aggrey Morris, wakati Shomary Kapombe na Leonel Saint-Preux walikosa.
Azam FC jana iliwaonyesha Watanzania kwamba inaweza kuwaadhibu Merreikh Jumapili Chamazi, baada ya kupata ushindi mnono katika Ligi Kuu wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar Chamazi.
Kiungo Frank Domayo alifunga mabao mawili sawa na mshambuliaji Kipre Tchetche, wakati bao lingine lilifungwa na Didier Kacumbangu. Baada ya mchezo huo, Azam imerejea kambini kwake, katika hosteli za Azam Complex, kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Jumapili.
Wakati huo huo: Wapinzania wa Yanga SC, BDF XI wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo pia kuelekea mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho la Afrika Jumamosi.
Yanga SC watacheza na BDF XI Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho wakihitaji ushindi mzuri kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano baadaye Gaborone.
Yanga SC imeweka kambi katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo huku ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa.
Refa wa mchezo huo atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.

0 comments:
Post a Comment