// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DRFA YAZIPA ‘TANO’ AZAM NA YANGA KUCHAPA WAPINZANI AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DRFA YAZIPA ‘TANO’ AZAM NA YANGA KUCHAPA WAPINZANI AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 16, 2015

    DRFA YAZIPA ‘TANO’ AZAM NA YANGA KUCHAPA WAPINZANI AFRIKA

    Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
    CHAMA cha Soka Dar es salaam (DRFA), kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya klabu barani Afrika, Azam FC na Yanga SC, kwa kuanza na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.
    Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini, baada ya kuifunga mabao 2-0 timu BDF XI ya Botswana, mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.
    Amisi Tambwe (katikati) aliifungia mabao yote mawili Yanga SC ikiichapa 2-0 BDF Jumamosi

    Kwa upande wa Azam FC, wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Cpmplex Chamazi.
    Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo, amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri waliyoanza nayo na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha, ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.
    Kasongo,pia amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DRFA YAZIPA ‘TANO’ AZAM NA YANGA KUCHAPA WAPINZANI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top