MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Emmanuel Adebayor alikuwa anajiandaa kuondoka klabu hiyo katika siku ya mwisho ya usajili, lakini ajabu mpango wake ulikwama dakika za mwisho.
Adebayor alikuwa anajiandaa kuhamia West Ham, lakini Spurs ikatangaza kwamba dili hilo limeshindikana na mchezaji huyo anabaki.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 30 amepoteza namba kawenye kikosi cha kwanza cha Spurs chini ya kocha Mauricio Pochettino, na amefunga mabao mawili katika mechi 15 msimu huu.
West Ham ilikuwa tayari kumchukua mshambuliaji huyo wa Togo kwa mkopo kutoka White Hart Lane, lakini ajabu dili hilo likafa dakika za mwishoni kabla ya dirisha dogo la usajili England kufungwa.
Dili la Emmanuel Adebayor kuhamia West Ham kutoka Tottenham limebuma
0 comments:
Post a Comment