// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 21, 2015

    CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND

    CHELSEA imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley Uwanja wa Stamford Bridge jioni ya leo. 
    Branislav Ivanovic alifunga bao lake la pili wiki kwa kikosi cha Jose Mourinho dakika ya 14 kuipatia Chelsea bao la kuongoza, kabla ya mchezaji mwenzake, Nemanja Matic kutolewa kwa kadi nyekundu.
    Matic alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumrudishia kipigo Ashley Barnes aliyemchezea rafu dakika ya 70.
    Beki wa pembeni wa Burnley, Ben Mee aliisawazishia timu yake dakika ya 81.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Zouma, Terry, Luis/Drogba dk85, Fabregas, Matic, Cuadrado/Willian dk63, Oscar/Ramires dk72, Hazard na Costa.
    Burnley; Heaton, Trippier, Shackell, Keane, Mee, Boyd, Jones, Arfield, Kightly/Vokes dk79, Barnes na Ings.
    Chelsea midfielder Cesc Fabregas catches Burnley's Kieran Trippier in the face with his arm during a challenge
    Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas akimkaba mchezaji wa Burnley, Kieran katika mchezo wa leo

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2963036/Chelsea-1-1-Burnley-Ben-Mee-cancels-Branislav-Ivanovic-strike-Nemanja-Matic-sees-red-Blues-dealt-title-blow.html#ixzz3SP4Kqrzq 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top