CHELSEA imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ugenini na wenyeji PSG katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na magwiji David Beckham, Sir Alex Ferguson na Michel Platini Uwanja wa Parc des Princes, beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic ndiye aliyeifungia bao hilo la ugenini timu yake dakika ya 36, ambalo lilikuwa na kuongoza kabla ya mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani kusawazisha dakika ya 54.
Sasa kikosi cha Jose Mourinho kimejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele iwapo kitashinda nyumbani au hata kutoa sare ya bila kufungana, kwani kitalindwa na bao la ugenini.
Chelsea wataikaribisha PSG katika mchezo wa marudiano Machi 11, Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian/Cuadrado dk79, Fabregas/Oscar dk83, Hazard na Diego Costa/Remy dk81.
PSG; Sirigu, Van der Wiel, Marquinhos, Thiago Silva, Maxwell, Verratti, David Luiz, Matuidi, Lavezzi/Pastore dk81, Ibrahimovic na Cavani.
Branislav Ivanovic akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Chelsea jana Ufaransa
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2957598/PSG-1-1-Chelsea-Branislav-Ivanovic-scores-crucial-away-goal-Jose-Mourinho-s-slender-advantage.html#ixzz3S3N4eCct
0 comments:
Post a Comment