CHELSEA imetanua mabawa kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Villa Park.
Eden Hazard aliifungia bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Jores Okore kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48.
Shujaa wa ushindi wa The Blues leo alikuwa ni
Branislav Ivanovic, aliyefunga bao la pili dakika ya 66.
Kiungo mpya, Juan Cuadrado alitokea benchi kwenda kumbadili Willian dakika ya 80, huo ukiwa mchezo wa kwanza baada ya kusajiliwa Jumatatu.
Ushindi huo, unaifanya Chelsea iongoze Ligi Kuu England kwa pointi saba zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City waliolazimishwa sare na Hull City nyumbani leo.
Kikosi cha Aston Villa; Guzan, Okore, Clark, Hutton, Cissokho, Cleverley/Sinclair dk74, Westwood, Delph, Gil, Agbonlahor/Benteke dk68 na Weimann/Cole dk80.
Chelsea; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian/Cuadrado dk80, Oscar/Mikel dk73, Hazard na Drogba/Remy dk64.
Willian (kulia) akipangusa viatu vya Ivanovic (katikati) kumpongeza baada ya kuifngia bao la ushindi Chelsea dhidi ya Villa leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2943899/Aston-Villa-1-2-Chelsea-Eden-Hazard-Branislav-Ivanovic-Blues-win.html#ixzz3R57UP1dS
0 comments:
Post a Comment