TIMU ya taifa ya Ivory Coast, imetinga Nusu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa mabao 3-1 Algeria usiku huu Uwanja wa Malabo, Equatorial Guinea.
Wilfried Bony alifunga bao la kwanza dakika ya 24, kabla ya Algeria kusawazisha kupitia kwa El Arabi Soudani mapema kipindi cha pili, dakika ya 51.
Lakini Bony tena akamlizia mpira wa adhabu uliopigwa na Yaya Toure dakika ya 69 kuipatia Ivory Coast bao la ushindi.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho akahitimisha ushindi wa Tembo kwa bao la tatu dakika ya 90.
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa; Gbohouo, Aurier, Bailly, Toure, Kanon, Tiene/Diomande dk67, Gradel, Toure, Serey Die, Gervinho na Bony/Tallo dk90.
Algeria: M'Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Taider, Bentaleb, Feghouli, Brahimi, Mahrez/Slimani dk72 na Soudani/Belfodil dk72.
Wilfried Bony (kulia) akishangilia na wenzake akiwemo Serge Aurier (kushoto) mjini Malabo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2935464/Ivory-Coast-3-1-Algeria-AFCON-2015-Wilfried-Bony-scores-twice-Elephants-progress.html#ixzz3QX5GXUDu
0 comments:
Post a Comment