BONDIA Francis Boniface Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na faini ya Sh. Milioni 1, baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa Meneja wa Baa yake ya Vijana Social mkoani Morogoro.
Cheka amepewa hukumu hiyo leo na moja kwa moja kwenda kuanza kutumikia kifungo chake jela. Cheka, aliyezaliwa Aprili 15, mwaka 1982 mjini Dar es Salaam, kwa sasa ni bingwa wa dunia wa taji la WBF uzito wa Super Middle.
Francis Cheka wa pili kulia akiwa kwenye gari la Polisi kwa safari ya gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo chake |
Cheka anakwenda jela akiwa bingwa wa dunia wa taji la WBF uzito wa Super Middle
Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo, Cheka alidai kwamba sababu halisi ya kifungo ni fitina za viongozi wa mkoa wa Morogoro baada ya kudai zawadi yake aliyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete ya bati.
Cheka aliwaambia Waandishi wa Habari akiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa gerezani kwamba, kilichomponza hadi kufungwa leo ni kudai bati alizoahidiwa na Rais Kikwete.
0 comments:
Post a Comment