ARSENAL imeadhibiwa nyumbani Uwanja wa Emirates, baada ya kufungwa mabao 3-1 na Monaco ya Ufaransa katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Maana yake, Arsenal wanatakiwa kwenda kushinda 3-0 ugenini ili kufuzu Robo Fainali baada ya kipigo cha usiku huu.
Geoffrey Kondogbia alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Arsenal inayofundishwa na Arsene Wenger dakika ya 38, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Dimitar Berbatov kufunga la pili dakika ya 53.
Alex Oxlade Chamberlain akaifungia The Gunners dakika ya 90+1, lakini But Yannick Ferreira-Carrasco akaifungia Monaco bao la tatu dakika ya 90+4.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin/Oxlade-Chamberlain dk68, Cazorla/Rosicky dk82, Sanchez, Ozil, Welbeck na Giroud/Walcott dk60.
Monaco; Subasic, Toure, Wallace Santos, Abdennour, Echiejile, Dirar/Kurzawa dk82, Kondogbia, Fabinho, Joao Moutinho, Martial/Bernardo Silva dk84, Berbatov/Ferreira-Carrasco dk76.
Mshambuliaji wa zamani Spurs, Manchester United na Fulham, Dimitar Berbatov akishangilia baada ya kuwafunga Arsenal
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2969294/Arsenal-1-3-Monaco-Dimitar-Berbatov-twists-knife-Geoffrey-Kondogbia-shows-Arsene-Wenger-just-s-missing.html#ixzz3SoOHN8UH
0 comments:
Post a Comment