// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BDF WATUA USIKU NA ‘MIKWARA MBUZI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BDF WATUA USIKU NA ‘MIKWARA MBUZI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 13, 2015

    BDF WATUA USIKU NA ‘MIKWARA MBUZI’

    Na Prince Akbark, DAR ES SALAAM
    KIKOSI kamili cha BDF ya Botswana kimewasili usiku wa jana tayari kwa kuwavaa Yanga, lakini kocha wao ametamka kwamba hawakuja kutalii.
    Kikosi hicho kilicholetwa na dege maalum la jeshi kimewasili usiku wa jana majira ya saa 2 usiku na kupokelewa na wenyeji wao pamoja na maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Mara baada ya kutua kocha wa timu hiyo Letang Kgengwenyane ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba wamekuja kupambana kiukweli na Yanga na hawakuja kushangaa nchini Tanzania.
    "Tunashuru tumefika salama, nawajua Yanga lakini ninachoweza kusema kwasasa ni kwamba tupo tayari kwa mchezo hatukuja kama watalii hapa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BDF WATUA USIKU NA ‘MIKWARA MBUZI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top