TIMU ya Barcelona imeifunga mabao 3-1 Villarreal katika Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme, maarufu Copa del Rey usiku huu Uwanja wa Nou Camp.
Ushindi huo wa 10 mfululizo katika mashindano yote kwa vigogo hao wa Hispania ulitokana na mabao ya Lionel Messi, Andres Iniesta na Gerard Pique.
Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Muargentina Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 41, kabla ya Villarreal kusawazisha kupitia kwa Manu Trigueros dakika ya 48.
Andres Iniesta akaifungia Barcelona bao la pili dakika tatu baadaye kabla ya Gerard Pique kukamilisha ushindi wa 3-1 dakika ya 65.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Ter Stegen, Alves, Pique, Mathieu, Alba, Rafinha/Rakitic dk69, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar.
Villarreal: Asenjo, Mario, Musacchio, Victor Ruiz, Costa, Jonathan dos Santos, Pina, Bruno/Trigueros dk33, Cheryshev/Gomez dk74, Giovani dos Santos/Rukavina dk52 na Vietto.
Wachezaji wa Barcelona wakifurahia ushindi wao dhidi ya Villarreal Uwanja wa Nou Camp katika Nusu Fainali ya Copa del Rey
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2949668/Barcelona-3-1-Villarreal-Lionel-Messi-Andres-Iniesta-Gerard-Pique-strike-Copa-del-Rey-semi-final-leg.html#ixzz3RTZpnMYd
0 comments:
Post a Comment