LIVERPOOL imeiachapa Tottenham Hotspur mabao 3-2 usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfeld.
Wekudu hao walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Lazar Markovic dakika ya 15, kabla ya Tottenham kusawazisha kupitia kwa Harry Kane dakika ya 26, hilo likiwa bao lake la 13 katika ligi msimu huu.
Hosts wakapata bao la pili kupoitia kwa Nahodha Steven Gerrard aliyefunga kwa penalti dakika ya 53, kabla ya Mousa Dembele kuisawazishia Liverpool dakika ya 61.
Mshambuliaji Mario Balotelli aliyetokea benchi akaifungia Liverpool bao la ushindi dakika ya 83 na sasa Wekundu wa Anfield wanabaki nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zao 43, moja nyuma Tottenham walio nafasi ya sita.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can 6, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson, Gerrard/Lovren dk67, Moreno, Coutinho, Markovic/Lallana dk79 na Sturridge/Balotelli dk73.
Tottenham; Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Mason/Paulinho dk69, Lamela, Dembele/Soldado dk85, Eriksen/Chadli dk81 na Kane.
Mario Balotelli hakuwa na makeke baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Tottenham
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2948157/Liverpool-3-2-Tottenham-Mario-Balotelli-Reds-hero-scores-Premier-League-goal-club-late-on.html#ixzz3RP8w8OvF
0 comments:
Post a Comment