AZAM FC imemaliza ziara yake ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bila ushindi baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 Don Bosco ya Kinshasa Uwanja wa TP Mazembe mjini humo.
Mechi iliyopita, Azam FC inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog, ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 ma ZESCO United ya Zambia mabao yake yakifungwa na kiungo Frank Domayo.
Katika mchezo wa kwanza, mabingwa hao wa Tanzania Bara, walifungwa 1-0 na wenyeji wao, TP Mazembe.
Azam FC iliyokwenda huko kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan katikati ya mwezi huu, itarejea nchini kesho baada ya wiki moja ya kuwa Lubumbashi.
Katika mchezo wa kwanza leo, TP Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, iliwafunga 1-0 ZESCO United wenye mshambuliaji Mtanzania pia, Juma Luizio.
Mazembe imefunga timu zote katika mashindano hayo ya mfumo wa Ligi, baada ya kuifunga Don Bosco mabao 3-1.

0 comments:
Post a Comment