// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAILIPUA MERREIKH 2-0 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAILIPUA MERREIKH 2-0 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 15, 2015

    AZAM FC YAILIPUA MERREIKH 2-0 CHAMAZI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imeanza vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Awali jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo, uliohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick, hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu.
    Kavumbangu alifunga bao hilo dakika ya tisa baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa Salim Magoola kufuatia yeye mwenyewe kuunganisha krosi ya Brian Majwega.
    Mfungaji wa bao la kwanza la Azam FC, Didier Kavumbangu kulia akishangilia na wenzake, Erasto Nyoni na Frank Domayo kushoto
    Didier Kavumbangu akiwa hewani kupiga mpira kichwa dhidi ya beki wa Merreikh, Kamal Amir
    Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche alifanikiwa kumpiga chenga wa Merreikh, Salim Magoola na kutia krosi, ambayo ilikosa muunganishaji

    Azam FC ingeweza kurejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya dakika 45 za kwanza ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0, kama washambuliaji wake Kipre Tchetche na Kavumbagu wangetumia nafasi mbili zaidi nzuri walizopata. 
    Kipindi cha pili, Azam FC iliendelea kucheza vizuri ikishambulia na kujilinda vizuri kutowapa nafasi wapinzani kupata bao la ugenini.
    Hata hivyo, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kavumbangu kila mmoja alikosa bao la wazi.
    Nahodha wa Azam FC, John Raphael Bocco aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche aliifungia timu yake bao la pili dakika ya 70 kwa kichwa baada ya shambulizi lililoanzishwa na Majwega.
    El Merreikh walilainika baada ya bao hilo na kama Azam FC wangekuwa makini wangepeta japo bao moja zaidi.
    Azam FC sasa inahitaji kwenda kuulinda ushindi huo ugenini wiki ijayo ili kwenda hatua ya 32 ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikishiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mwaka huu.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Serge Wawa, Kipre Balou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo/Himid Mao dk58, Didier Kavumbangu/Amri Kiemba dk88, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
    El Merreikh; Salim Magoola, Kamal Amir, Gaffar H Ali/Mohammed Traore dk46, Elrayah Maki, Babeker Bakri, Kartokaila Balla, Mussa Mussab, Abdallah Ragei, Solomon Jobson, Sharif Ramadhan na Allan Wanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAILIPUA MERREIKH 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top