Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Tanzania Bara, Azam FC leo wanaanza kampeni yao ya kuwania taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa, ni marudio ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Agosti 20, mwaka jana Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.
Dakika 90 ziliisha timu hizo zikiwa hazijafungana na katika mikwaju ya penalti Merreikh waliing’oa Azam FC kwa 4-3 na kwenda Nusu Fainali, baadaye Fainali hatimaye wakabeba Kombe.
Lakini siku hiyo, Azam FC ilipata pigo kubwa, mshambuliaji wake, John Bocco aliumia kipindi cha kwanza na kutolewa- na akakaa nje hadi Januari alipoanza kurudi taratibu baada ya kutibiwa hadi Afrika Kusini.
Siku Merreikh wanaitoa Azam FC Rwanda, safu yao yao ya ulinzi ilikuwa inaongozwa na beki kutoka Ivory Coast, Serge Wawa Pascal. Lakini leo, mlinzi huyo atatokea kwenye vyumba vya Azam FC.
Azam FC iliikosa kidogo kidogo tu saini ya mshambuliaji wa Mali, Mohammed Traore ambaye mwenyewe hadi kesho anapenda kuhamia Dar es Salaam.
Mshambuliaji Mkenya, Alan Wanga ni mchezaji mwingine ambaye yuko tayari kusaini Azam FC wakati wowote sawa na kipa Salim Magoola.
Hali ya wachezaji wa Merreikh kuipenda Azam FC imefanya viongozi wa klabu hiyo vigogo wa Sudan waanze kidogo kutoifurahia timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
Zaidi ya hayo, kila timu imeboresha benchi lake la Ufundi baada ya kukutana Agosti- Azam FC ikimuongeza Mganda George ‘Best’ Nsimbe aliyekuwa kocha wa KCCA ya Uganda iliyoitoa Merreikh mwaka jana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu ya matajiri wamiliki visima vya mafuta Sudan chini ya Rais wake, Gamal Al-Wali nayo imemchukua kocha mzoefu Afrika, Mjerumani Otto Pfister ambaye mwaka 1992 alishinda tuzo ya Kocha Bora Afrika.
Pfister amefundisha timu za taifa za Burkina Faso, Zaire, Cameroon, na Ghana na amefika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, akiwa na Cameroon na Ghana. Pfister aliyetwaa Kombe la Dunia la U-17 akiwa Ghana, pia ametwaa Kombe la Mataifa ya Afrika la U19 akiwa na Ivory Coast kabla ya kuiongoza Togo kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2006.
Pfister pia aliiwezesha Saudi Arabia kufuzu Kombe la Dunia mwaka 1998 na ameshinda mataji ya Ligi za Misri na Lebanon na vikombe kaadhaa Tunisia, Misri, Lebanon na Sudan.
Kwa ujumla mchezo wa leo kati ya Azam FC na Merreikh unatarajiwa kuwa mtamu sana, na wengi wanasema hii ni mechi ambayo hadhi yake imezidi kuwa ya hatua ya mchujo. Hii ni mechi yenye hadhi ya hatua ya 32 Bora.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 11:00 jioni na tiketi zitaanza kuuzwa asubuhi ya leo. Burudani Chamazi leo.

Kikosi cha Azam FC kinachotarajiwa kumdnyana na El Merreikh leo |

0 comments:
Post a Comment