WASHIKA Bunduki, Arsenal wamezinduka baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Leicester City usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Laurent Koscielny dakika ya 27 akimalizia kona ya Mesut Ozil na Theo Walcott dakika ya 41.
Bao pekee la Leicester lilifungwa na Andrej Kramaric.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Rosicky, Walcott/Ramsey dk73, Cazorla, Ozil na Sanchez/Giroud dk68.
Leicester; Schwarzer, Huth, Upson/Wasilewski dk59, Morgan, Simpson, Konchesky, James, Cambiasso, Mahrez, Schlupp na Kramaric.
Theo Walcott akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Arsenal dhidi ya Leicester
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2948266/Arsenal-2-1-Leicester-City-match-report-Laurent-Koscielny-Theo-Walcott-strike-Gunners.html#ixzz3RPBM8Rp6
0 comments:
Post a Comment