ARSENAL imewapa zawadi nzuri mashabiki wake ya kuanzia mwezi mpya, baada ya kuichapa mabao 5-0 Aston Villa Uwanja wa Emirates jioni ya leo.
Olivier Giroud alifunga bao la kwanza dakika ya nane akimalizia kazi nzuri ya Mesut Ozil
Ozil alifunga bao likakataliwa kipindi cha kwanza kabla ya kufunga lingine lililokubaliwa dakika ya 56.
Theo Walcott akafunga bao la tatu dakika ya 64, Santi Cazorla la nne dakika ya 75 na Hector Bellerin la tano dakika ya 90. Mchezaji mpya,
Gabriel alikuwa kwenye benchi la The Gunners.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Kosceilny, Monreal, Coquelin, Aaron Ramsey/Flamini dk77, Theo Walcott/Rosicky dk70, Santi Cazorla, Mesut Ozil na Olivier Giroud/Akpom dk70.
Aston Villa; Guzan, Hutton, Clark, Okore, Richardson, Sanchez/Westwood dk76, Delph, Cleverley/Agbonlahor dk66, Gil, Weimann/Sinclair dk66 na Benteke.
Ozil akishangilia baada ya kuifungia Arsenal katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Aston Villa leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2935220/Arsenal-5-0-Aston-Villa-Mesut-Ozil-Olivier-Giroud-Theo-Walcott-Santi-Cazorla-Hector-Bellerin-score.html#ixzz3QVghp47C
0 comments:
Post a Comment