ARSENAL imetinga Robo Fainali ya Kombe la FA, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Middlesbrough jioni hii Uwanja wa Emirates.
Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud alifunga bao la kwanza dakika ya 27 na pili sekunde 135 baadaye.
Alexis Sanchez na Danny Welbeck wote walikaribia kufunga na Theo Walcott pia aliyeingia kuchukua nafasi ya Welbeck dakika ya 72, naye alikosa bao la wazi.
Gabriel Paulista aliichezea kwa mara ya kwanza Arsenal na kuonyesha uwezo mzuri. Droo ya Robo Fainali ya Kombe la FA inapangwa kesho Saa 1.35 usiku, kabla ya mchezo wa Preston na Manchester United.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Chambers, Gabriel, Koscielny, Gibbs, Cazorla, Flamini, Sanchez/Rosicky dk72, Ozil, Welbeck/Walcott dk72 na Giroud/Akpom dk83.
Middlesbrough: Mejias, Fredericks, Omeruo, Gibson, Friend, Clayton, Leadbitter, Adomah, Tomlin/Vossen dk54, Bamford/Reach dk54 na Garcia.
Giroud akishangilia baada ya kufunga leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2954574/Arsenal-2-0-Middlesbrough-Olivier-Giroud-double-sees-Arsene-Wenger-s-men-avoid-upset-reach-FA-Cup-quarter-final.html#ixzz3RqH8P665
0 comments:
Post a Comment