// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AMINI USIAMINI, REAL MADRID WAWATAKA HASSAN ISIHAKA NA SINGANO MESSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AMINI USIAMINI, REAL MADRID WAWATAKA HASSAN ISIHAKA NA SINGANO MESSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 02, 2015

    AMINI USIAMINI, REAL MADRID WAWATAKA HASSAN ISIHAKA NA SINGANO MESSI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Real Madrid Castilla, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Hispania, maarufu kama Segunda B inataka wachezaji wawili wa SImba SC, beki Isihaka Hassan na kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’.
    BIN ZUBEIRY inafahamu timu hiyo ya pili ya mabingwa wa Ulaya, Real Madrid inayocheza mechi zake Uwanja wa Alfredo di Stefano, kupitia mwakilishi wake, Rayco Garcia imewasilisha rasmi maombi yake kwa klabu ya Simba SC juu ya wachezaji hao.
    Garcia amesema anawataka wawili hao Juni mwaka huu waende Hispania kufanyiwa majaribio katika timu hiyo na kama wakifuzu wataanza maisha mapya Ulaya.
    Garcia aliwaona wachezaji hao Jumatano iliyopita wakati Simba SC ikicheza na Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
    Nahodha wa Simba SC, Hassan Isihaka anatakiwa na Real Madrid ya Hispania 

    Garcia alikuwa nchini kwa ajili ya kusaini Mkataba na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa kujenga kituo cha michezo kwa ajili ya kuzalisha vipaji. 
    Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo wa miaka 18, Dar es Salaam wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema ujenzi huo utagharimu Sh Bilioni 16 na unatarajiwa kuanza Mei mwaka huu na kwamba utakamilika baada ya miezi 18.
    Dk Dau alisema kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye kijiji cha michezo cha shirika hilo (NSSF Sports City), kitakuwa eneo la Mwasonga, Kigamboni, Dar es Salaam. 
    “Tuna eneo la zaidi ya ekari 400 ambapo tutajenga viwanja, shule ya michezo, nyumba za kuishi na maduka. Lengo letu tuzalishe na kuuza wachezaji. Tunakusudia kuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 13, 18, 20, timu B na timu ya wakubwa,” alisema Dk Dau. 
    Royco kulia akitiliana saini na Dk Dau kushoto Mkataba wa ujenzi wa akademi ya kisasa Mwasonga, Kigamboni, Dar es Salaam

    Alisema utekelezaji wa kituo hicho utaanza hivi karibuni kwa kutumia majengo ya kukodi wakati wakisubiri ujenzi kukamilika.“Hivi hapa baada ya kusaini mkataba, utekelezaji utaanza kwa kutumia majengo ya kukodi ambayo tunadhani yatakuwa maeneo ya Temeke na tutakuwa tukitumia viwanja vya Karume na Uhuru,” alisema. 
    Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF alisema katika kuendesha kituo hicho, kila kitu kitafanywa na Real Madrid kuanzia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu. 
    “Sisi tunachukulia huu mradi ni uwekezaji na hatufanyi hisani, itazingatia misingi ya biashara na faida kubwa ni kwamba NSSF itaongeza kipato, lakini pia kituo kitatumika kuitangaza Tanzania kwa sababu yatakayofanyika yataonyeshwa kwenye Televisheni ya Real Madrid,” alifafanua Dk Dau. 
    “Lakini pia wakati umefika sasa kwa Tanzania kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022, kama unaandaa vizuri vijana wa miaka 13 sasa mpaka mwaka 2020 wanaweza kuwakilisha vizuri kwenye mechi za kufuzu na mwaka 2022 wakashiriki Kombe la Dunia, wakikosa la Qatar, basi hata hizo zinazokuja, hiyo pia ni moja ya madhumuni ya kituo hicho.” 
    Akizungumzia namna walivyofikia uamuzi wa kujenga kituo, Dk Dau alisema wazo hilo lilipatikana Agosti mwaka jana na kisha likapelekwa kwenye Mkutano wa Wanachama uliofanyika Arusha ambako waliazimia NSSF iwekeze rasmi kwenye michezo kabla ya kuwasilishwa kwenye bodi na utekelezaji kuanza kufanyika. 
    “Tulitembelea sehemu nyingi kuona wenzetu wanafanyaje. Binafsi nilitembelea nchi kadhaa za Ulaya, nilienda kituo cha Manchester United, Sunderland, Real Madrid kwa hapa Afrika nilikwenda Asec Mimosas (Ivory Coast) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC) kuona wanafanyaje, ziara ikazaa matunda kwani tulikubaliana na Madrid na ndio wamekuja kusaini mkataba,” alifafanua Dk Dau. 
    Kwa upande wake, Garcia aliishukuru NSSF wa kuwa na mpango huo na kuahidi kufanya kazi ili kuipatia Tanzania mafanikio. “Tukifanikiwa kuwatoa vijana hao, Tanzania itaweza kushiriki kwenye michuano mikubwa kama alivyosema Dk Dau, inabidi tufanye kazi ili vijana wafanikiwe, wafike mbali,” alisema Garcia. 
    Mbali na Garcia ambaye pia ni kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Madrid, wengine walioambatana kwenye msafara huo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, Ruben de la Red, Kocha Mkuu wa timu za vijana, Francisco Martin Ramos na Juan Jose San Roman Milla.
    Mradi huu ni matunda ya ziara ya kikosi cha magwiji wa Real Madrid waliozuru nchini Agosti mwaka jana wakiongozwa na Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Mreno Luis Figo na kucheza mechi ya kirafiki na wachezaji nyota wa zamani wa Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMINI USIAMINI, REAL MADRID WAWATAKA HASSAN ISIHAKA NA SINGANO MESSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top