// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ALLY CHOCKY NA ASHA BARAKA MNAHITAJIANA SANA ILA NI UJEURI WENU TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ALLY CHOCKY NA ASHA BARAKA MNAHITAJIANA SANA ILA NI UJEURI WENU TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, February 16, 2015

    ALLY CHOCKY NA ASHA BARAKA MNAHITAJIANA SANA ILA NI UJEURI WENU TU

    Kama kuna kipindi ambapo Asha Baraka na Twanga Pepeta yake inamhitaji Ally Chocky basi ni sasa kuliko kipindi chochote kile, lakini ukimuuliza Asha Baraka jambo hilo atakuambia hakuna kitu kama hicho.
    Na kama kuna kipindi ambacho Ally Chocky anaihitaji Twanga Pepeta ya Asha Baraka basi ni sasa kuliko kipindi chochote kile katika historia yake ya kimuziki, lakini nae ukimuuliza atakuambia Twanga Pepeta kwa muda huu haipo akilini mwake.
    Kwasasa habari ya mjini ni safari ya Ally Chocky kurudi Twanga Pepeta, kila mtu amekuwa fundi wa kutoa tetesi anazozijua. Mara tunaambiwa show ya mwisho ya Ally Chocky kwa Extra Bongo ni iliyofanyika juzi (Siku ya Wapendanao) pale Landmark Hotel Ubungo.

    Kwamba Chocky anasafiri kwenda nje ya nchi kwa siku kadhaa, akirejea Bongo ni Twanga Pepeta moja kwa moja – eti Chocky anakwenda nje na kuwaachia bendi wanamuziki wake waiendeshe kwa siku zote atakazokuwa hayupo akiamini kuwa watashindwa na hiyo itakuwa sababu nzuri kwake ya kuivunja bendi yake. Tetesi ya kwanza hiyo.
    Tetesi nyingine inasema Chocky atakapotua Twanga Pepeta basi kuna wasanii kadhaa watapigwa panga ili kutoa nafasi kwa wasanii wapya atakaokwenda nao Twanga. Masikini ya Mungu sijui kama wale Wacongo wake mahiri kwenye magitaa waliotambushwa kwa kishindo watapata nafasi ya kwenda Twanga au ndio safari ya kurejea kwao itakuwa imewadia. 
    Lakini pia ipo tetesi inayosema Chocky anarejea Twanga kama mwanahisa – kwamba atapewa hisa kwenye bendi na hatakuwa mwajiriwa kama ilivyokuwa kwenye vipindi vyake viwili alivyowahi kuitumikia Twanga Pepeta.
    Hali si shwari kabisa ndani ya kambi ya Twanga Pepeta, baadhi ya wanamuziki wamekubwa na hofu, wako wasiokubali kabisa ujio wa Chocky wakiamini kuwa mwimbaji huyo si mwarobaini wa kuirejesha Twanga kileleni, ipo shaka kubwa juu ya Chocky kukosa ushirikiano kutoka kwao kama kweli atarejea Aset.
    Ikumbukwe mwaka 2006 Chocky aliporejea Twanga Pepeta kutoka Mchinga Generation alizua mgawanyiko mkubwa na kupelekea kuzaliwa kwa Twanga Chipolopolo iliyoundwa na wasanii ambao hawakuwa tayari kufanya kazi na Chocky akiwemo Banza Stone, Msafiri Diouf na Victor Nkambi.
    Kwa mazingira ya soko la muziki wa dansi kwa sasa, si rahisi tena mambo ya Twanga Chipolopo kujirudia ila ni wazi kuwa kutakuwepo mgomo baridi ambao unaweza kupekelekea baadhi ya wasanii kupoeteza vibarua vyao pindi tetesi za Chocky kurejea Twanga zikiwa kweli.
    Majuzi nilimuuliza Asha Baraka juu ya tetesi za Chocky kurejea Twanga, akaniambia hayo ni maneno ya mashabiki tu, hakuna kitu kama hicho, Asha akafafanua kuwa maneno hayo yamekuja baada ya wao kupatana lakini suala la msanii huyo kurejea Aset kwa sasa halipo.
    Kama Asha Baraka alikuwa ananificha basi bila shaka hiyo ni kwa faida yake ambayo anaijua yeye mwenyewe ila binafsi nimeyachukulia maneno yake kama kauli rasmi kutoka Aset ingawa maisha ya sanaa ni kama ya siasa – ukweli na uongo unatenganishwa na mstari mwembamba sana.
    Angalau kidogo Ally Chocky alinipa maneno yaliyonifanya niamini kuwa lolote linaweza kutokea. Chocky aliniambia hivi: “Sijui kwanini watu wanasumbuka sana kufuatilia maisha yangu, kila mtu anaongea lake. Mimi kama nikiamua kurudi Twanga hakuna wa kunizuia, nikiamua kuvunja Extra Bongo hakuna wa kunizuia, hata nikiamua kuacha muziki na kufanya shughuli zingine hakuna wa kunizuia kwa kuwa hayo ni mambo yangu binafsi na ni maisha yangu,” 
    Niseme jambo moja kwa Asha Baraka na naomba aniwie radhi kama nitakuwa nimemkosea. Twanga Pepeta imeyumba, imekosa tungo zenye mashiko,  Twanga Pepeta inakosa nidhamu ya kutosha miongoni mwa wasanii ndani na nje ya jukwaa, Twanga Pepeta bado haijampata mrithi wa marehmu Abuu Semhando aliyekuwa mkali kama pilipili pale linapokuja suala la uwajibikaji. Kwa sasa simuoni mwingine anayeweza kuyafunika yote hayo zaidi ya Ally Chocky na ndio maana nikasema kuwa kama kuna kipindi ambacho Asha Baraka anamhitaji Ally Chocky basi ni sasa kuliko kipindi chochote kile huko nyuma.
    Lakini pia niseme yafuatayo kwa Chocky: Biashara ya muziki wa dansi imekuwa ngumu, Extra Bongo inapata wakati mgumu kupenya kwenye soko hili gumu, gharama za uendeshaji bendi ni kubwa kuliko kinachoingia, licha ya kuwa uwezo wake bado ni mkubwa sana lakini mvuto wake wa kimuziki umepungua na unahitaji ‘kubustiwa’ – sehemu pekee inayomfaa kwa wakati huu ni Twanga Pepeta. Hakuna ubishi kuwa aling’ara zaidi akiwa Twanga Pepeta kuliko sehemu yoyote ile katika historia yake ya kimuziki si Lola Afrika, Bantu Group, Washirika, MK Beats, Doube Extra, Mchinga, TOT wala Extra Bongo na ndio maana nasema kama kuna kipindi ambacho Chocky anamhitaji Asha Baraka na Twanga Pepeta ni sasa kuliko kipindi chochote kile. Namuomba radhi pia kama nimemkosea.
    Sisemi kuwa Twanga Pepeta bila Chocky haiwezekani wala sisemi kuwa Chocky bila Twanga Pepeta haiwezekani, la hasha! ila nasema tu kuwa Asha Baraka na Chocky mnahitajiana sana kwa sasa lakini ni ujeuri wenu, najua mkiweka kando jeuri zenu (kama bado hamjaweka) basi tutashuhudia kitu kimoja kitakachopasua anga za muziki wa dansi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALLY CHOCKY NA ASHA BARAKA MNAHITAJIANA SANA ILA NI UJEURI WENU TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top