MTAALAMU wa soka maridhawa, Ronald Koeman ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Januari Ligi Kuu ya England baada ya kuiongoza Southampton kuvifunga vigogo, Arsenal na Manchester United.
Watakatifu wameshinda mechi zao zote tatu za Ligi Kuu ya England mwezi uliopita, ikiwemo dhidi ya Newcastle, na kubaki katika kinyang'anyiro cha Nne Bora.
Kwa sasa, Southampton inashika nafasi ya nne katika Ligi Kuu England, ikizidiwa pointi moja na Man United na ikiizidi pointi moja pia Arsenal.
Ronald Koeman ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Januari Ligi Kuu ya England baada ya kuiwezesha Southampton kushinda mechi tatu
0 comments:
Post a Comment