Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
AFRICAN Sports ya Tanga inatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho kwenda Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kurugenzi.
Kocha Msaidizi wa Sports, Kassim Muhaji Mwabuda amesema kwamba maandalizi ya safari yamekamilika na kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya mchezo huo.
Beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kwamba japokuwa wamekwishajihakikishia kucheza Ligi Kuu msimu ujao, lakini wataingia katika mchezo huo kwa nguvu zote ili washinde.
“Tunataka ushindi, tunakwenda Mafinga kwa ajili ya kupigania ushindi tu. Najua kwa sababu tumekwishapanda, watu wanaweza wakadhani tutakwenda kuwalgezea wapinzani wetu, hapana. Tunakwenda kukaza kupigania ushindi,”amesema Mwabuda.
Amesema wataondoka na kikosi chao kamili ambacho ni kinaundwa na Yussuf Abdul, Halfan Twenye, Mussa Ajiran, Juma Shemvuni, Mwaita Ngereza, Sultan Juma, Ramadhani Hamidu, Ally Ramadhani na Ally Shiboli.
Wengine ni James Mendi, Nyanda Kaziyoba, Tokala Nzau, Ayub Masoud, Ally Issa, Mussa Chambe, Ally Ahmed, Fadhili Kizenga, Evarstus Munjwahuki, Maulid Abbas, Nzara Ndaro, Rashid Ally, Hussein Issa, Zakaria Majaliwa, Issa Yassin, Paul Muna, Mohamed Rashid na Kassim Juma.
Sports imejihakikishia kurejea Ligi Kuu baada ya miaka 23, ikifikisha pointi 44 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Kundi A, ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Kurugenzi na Friends Rangers.

Kocha Msaidizi wa Sports, Kassim Mwabuda |

Wachezaji wa African Sports wakiwa mazoezini jana Uwanja wa sekondari ya Usagara, Tanga |
Sports imejihakikishia kurejea Ligi Kuu baada ya miaka 23, ikifikisha pointi 44 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Kundi A, ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Kurugenzi na Friends Rangers.
0 comments:
Post a Comment