Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
ZAIDI ya Shilingi Milioni 40 zimetengwa kama zawadi kwa washindi wa mbio za Kilimanaro Marthon zinazotarajiwa kufanyika Machi 1, 2015 mjini Moshi.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbali na washindi kujinyakulia zaidi ya shilingi milioni 40 pia watapata fursa ya kujishindia zawadi nyingine kabambe za kuvutia kutoka wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini shirikishi.
Alisema washindi wa mbio ndefu za marathon ya kilomita 42 watajishindia jumla ya shilingi milioni 20, na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio za walemavu zinazodhaminiwa na GAPCO wakijishindia kiasi cha shilingi milioni 6.
Addison alisema kuwa mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za nusu marathon (Tigo Kili Half Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu. Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio.
Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Tigo, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, , CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

0 comments:
Post a Comment