MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Yaya Sanogo amekamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Crystal Palace kumalizia sehemu iliyobaki ya msimu wa Ligi Kuu ya England.
Arsene Wenger aliwakatalia Bordeaux ya Ufaransa waliomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akacheze Selhurst Park, wakati Hull City na Queens Park Rangers nao pia walimtaka mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21.
Wenger anatumai Sanogo anaweza kupata uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya England anaouhitaji baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Palace chini ya kocha mpya, Alan Pardew tangu aondoke Newcastle United.
Mshambuliaji wa Arsenal, Yaya Sanogo akiwa na jezi ya Crystal Palace baada ya kukamilisha uhamisho wake wa mkopo
0 comments:
Post a Comment