BONDIA Mmarekani, Deontay Wilder amemuenzi vizuri bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, Muhammad Ali baada ya Alfajiri ya leo kutawazwa kuwa bingwa wa dunia uzito wa juu.
Hiyo inafuatia kumshinda Bermane Stiverne kwa pointi ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas na kutwaa taji la WBC akiwa Mmarekani wa kwanza kushinda taji la uzito wa juu duniani baada ya miaka zaidi ya nane.
Wilder, ambaye awali aliwakalisha ndani ya raundi ya tano wapinzani wake wote katika mapambano 32 yaliyopita, mara mbili alimpa kibano cha nguvu Stiverne, lakini hakufanikiwa kumpiga kwa Knockout mbabe huyo wa Haiti.
Mwishowe akashinda pointi za majaji wote, 118-109, 119-108 na 120-107 dhidi ya Wilder. Ni ushindi ambao umekuja katika usiku ambao mbabe wa kihistoria kuwahi kutokea katika ndondi za uzito wa juu, Ali alikuwa anasherehekea miaka 73 ya kuzaliwa kwake.
Stiverne akienda chini baada ya kibano cha Wilder, lakini alisimama na kuendelea na pambano
Wilder akimchapa Stiverne aliyeoonyesha usugu wa kukomaa na kumaliza pambano
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2915193/Deontay-Wilder-crowned-heavyweight-world-champion-points-win-Bermane-Stiverne.html#ixzz3P9YYvsde
0 comments:
Post a Comment