TIMU ya West Ham United imeitoa kwa penalti 9-8 Everton katika mchezo wa marudio wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA usiku wa Jumanne Uwanja wa Upton Park, kufuatia sare ya 2-2.
Enner Valencia aliifungia bao la kwanza The Hammers dakika ya 56, kabla ya winga wa Toffees, Aiden McGeady kutolewa kwa kadi ya pili.
Kevin Mirallas aliyetokea benchi, aliisawazishia Everton pungufu dakika ya 82 kabla ya Romelu Lukaku kufunga bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 97. Hata hivyo, mtokea benchi mwingine, Carlton Cole akaisawazishia West Ham dakika ya 113.
Sifa zimuendee kipa wa Hammers, Adrian aliyefunga penalty ya mwisho na sasa West Ham watamenyana na Bristol City katika Raundi ya Nne wikiendi ya Januari 24 na 25.
Kipa Adrian akishangilia baada ya kufunga penalti ya mwisho ya West Ham katika ushindi wa 9-8 dhidi ya Everton
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2908979/West-Ham-2-2-Everton-9-8-pens-Keeper-Adrian-scores-winner-penalty-shootout-snuff-10-men-Toffees-comeback-FA-Cup.html#ixzz3OkLmuRAE
0 comments:
Post a Comment