KLABU ya West Bromwich Albion imefungua milango ya mauzo ya Saido Berahino mwezi huu, huku Tony Pulis wakitarajiwa kuimarisha kikosi chao kuepuka kushuka Daraja.
Mwenyekiti wa klabu, Jeremy Peace awali alisema kwamba mchezaji huyo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya England hataondoka The Hawthorns, lakini baada ya kuwasili kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Terry Burton amekuja na mipango mipya.
Liverpool na Tottenham zinamfuatilia mchezaji huyo zikiwa zinamuhitaji, ingawa bado hazijatoa ofa, huku Burton akisema mkali huyo wa mabao atapatikana kwa Pauni Milioni 20.
West Brom imesema inamuuza kwa Pauni Milioni 20 Saido Berahino
0 comments:
Post a Comment