// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 27, 2015

    WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    WASHINDI wa Copa Coca-Cola 2014 wamekabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwa mdhamini wa michuano hiyo ya umri chini ya miaka 15 kwa wavulana na wasichana kampuni ya Coca-Cola. Fedha hizo kwa washindi mbalimbali tayari zimeingizwa kwenye akaunti zao.
    Kwa upande wa wavulana; washindi na kiwango walichopata ni mabingwa Dodoma (sh. milioni nane), makamu bingwa Kinondoni (sh. milioni tano), mshindi wa tatu Kigoma (sh. milioni tatu) wakati timu yenye nidhamu Tanga (sh. milioni moja).
    Mchezaji bora Mwami Ismail kutoka Kigoma (sh. 500,000), mfungaji bora Timoth Timoth wa Dodoma (sh. 500,000), kipa bora Kelvin Deogratia wa Geita (sh. 500,000) na mwamuzi bora Abdallah Mbarome kutoka Zanzibar sh. 500,000).
    Kwa upande wa wasichana ni mabingwa Kinondoni (sh. milioni tano), makamu bingwa Ilala (sh. milioni tatu), mshindi wa watatu Temeke (sh. milioni mbili) wakati timu yenye nidhamu Mbeya imepata sh. milioni moja).
    Zubeda Mohamed wa Kinondoni ambaye ndiye mchezaji bora amepata sh. 500,000, mfungaji bora Stumai Abdallah wa Temeke sh. 500,000 wakati kipa bora ni Suleta Saad wa Zanzibar sh. 500,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top