KIPA Victor Valdes anatarajiwa kuanza kuidakia Manchester United katika mchezo wa Kombe la FA Raundi ya Nne dhidi ya Cambridge United Ijumaa usiku Uwanja wa Abbey.
Mlinda mlango huyo wa zamani wa Barcelona, aliyeshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia, atawadakia Mashetani Wekundu kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo dhidi ya timu hiyo ya Daraja la Pili, kwenhye Uwanja wa mashabiki 8,100.
Valdes, aliyezaliwa miaka 33 iliyopita, amesaini Mkataba wa miezi 18 Old Trafford mapema mwezi huu na alikuwa benchi katika mechi za Ligi Kuu ya England dhidi ya QPR na Southampton, kama kipa wa akiba wa David de Gea.
Victor Valdes anajiandaa kuidakia Manchester United dhidi ya Cambridge katika Raundi ya Nne Kombe la FA
0 comments:
Post a Comment