KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal anaamini kipa David de Gea atasaini Mkataba mpya katika klabu hiyo.
De Gea yuko kwenye mazungumzo na United juu ya kuongeza Mkataba ambao umebakiza miezi 18.
Wakati Real Madrid ikimtaka kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 arejee Hispania, United wiki hii imemsajili kipa mzoefu, Victor Valdes kama msaidizi wake, japokuwa mashabiki fulani wanahofu De Gea anaweza kuondoka.
Victor Valdes (kushoto) na David de Gea (kulia) wakifanya mazoezi na Manchester United jana jioni
Lakini alipoulizwa kama anafikiri kipa huyo atabaki, Van Gaal alisema jana: "Nafikiri hivyo, ndiyo. Nafikiri hakuna tatizo kwake kusaini. Ni sawa na wachezaji wengine. Unaweza kuniuliza kuhusu wachezaji wengine na nitakujivu hivyo hivyo.
Valdes atakuwa kwenye benchi wakati United inaikaribisha Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kesho Uwanja wa Old Trafford na Van Gaal anaamini ushindani wa namba baina ya Waspanyola hao wawili unaweza kuisaidia kuipeleka juu timu yake.
"Hakuna anayefurahi kuwa namba mbili,"amesema Van Gaal. "Anapaswa kuwa na dhamira ya kumpiku De Gea. Ambayo itakuwa ngumu sana kwake, lakini malengo yangu ni kuwa na wachezaji wazuri ambao wanaweza kushirikiana na kutufanya tuwe timu bora duniani,".
Van Gaal akimkabidhi Victor Valdes jezi ya Manchester United baada ya kusaini Mkataba wa miezi 18 kupiga kazi Old Trafford
0 comments:
Post a Comment