KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amemtetea mshambuliaji wa mkopo Radamel Falcao licha ya kwamba ameendelea kuboronga jana mjini London.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipoteza nafasi nne nzuri za kufunga, zikiwemo mbili akiwa amebaki yeye na nyavu.
Lakini licha ya hali hiyo kujirudia jana, kocha wa United, Van Gaal amesema; "Nafikiri alifanya vizuri,".
Kocha Mholanzi wa United ameongeza; "Si muhimu sana ninachofikiri, kwa sababu tunataka kufunga mabao. Na kwangu, natakiwa kuatazama alichezaji,".
"Kufungaa mabao ni jambo muhimu kwa mshambuliaji nafahamu, lakini kwangu ni jambo muhimu pia kama anashambulia. Na ninafikiri anafanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment