NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry ameanza kupanda milima ya kuelekea kuwa kocha, baada ya kwenda kupata mafunzo ya ukocha katika kozi ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) huko Wales.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye hivi karibuni alianza za uchambuzi wa mchezo wa soka katika Televisheni ya Sky Sports, hajafanya siri juu ya nia yake ya kuwa kocha.
Na harakati hizo zimeanza baada ya Henry kwenda Wales kupata kozi ya leseni B ya UEFA B.
Thierry Henry (kulia) akipeana mikono na Mkurugenzi wa timu ya taifa ya Wales, Osian Robertsbaada ya kumaiza kozi yake ya ukocha ya UEFA huko Wales
0 comments:
Post a Comment