BONDIA Floyd Mayweather kwa mara nyingine ameutikisa ulimwengu baada ya kuposti picha inayoonyesha mali na utajiri alionao.
mwanamichezo huyo anayeiingiza fehda nyingi zaidi kwa sasa duniani, ameposti picha kwenye mtandao akiwa amesimama mbele ya magari ya kifahari pamoja na ndege yake binafasi.
Mfalme huyo wa kutupa makode duniani aliyeiingiza Pauni milioni 66.1 kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka jana, katika picha hiyo ameambatanisha ujumbe usemao: "Karibu katika dunia yangu! Nani anataka kujitokeza na kucheza?'
Kutoka kushoto ni Ferrari 599 GTB Fiorano, Porsche 911 Turbo S, Lamborghini Aventador, Ferrari 458 Spider, Ferrari 458 Spider. Bugatti Grand Sport, Bugatti Veyron, Bugatti Veyron na ndege yake
0 comments:
Post a Comment